Jumapili 12 Oktoba 2025 - 13:53
Kwa ajili ya mfumo wa Kiislamu tunahitaji “Fiqhi ya Usalama” / Zaidi ya aya 500 ndani ya Qur’ani zinahusiana na Amani

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Ahmad Abidi, akirejelea tamko la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuhusu “Hawza inayoongoza na bora”, amesisitiza ulazima wa kujikita katika “Fiqhi ya kimfumo (Fiqh al-Nidhāmāt)”, hususan “Fiqhi ya Amani” ndani ya Hawza.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza mjini Isfahan Iran, Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Ahmad Abidi katika kikao maalumu kilichohudhuriwa na kundi la walimu wa ngazi za juu wa hawza, wajumbe wa sekretarieti ya Hawza inayoongoza na bora, na viongozi wa vitengo na taasisi za kielimu, alisisitiza nafasi ya kihistoria ya hawza katika kuitikia mahitaji ya zama, akasema:


“Hawza, kwa kutegemea hazina kubwa ya kielimu na historia yake tukufu, ina jukumu zito la kufafanua na kuweka misingi ya Fiqhi ya mfumo wa Kiislamu (Fiqh Nizām-sāz).” “Fiqhi ya Mifumo” ni miongoni mwa mahitaji makubwa katika jamii ya Kiislamu ya leo, akiongeza kuwa:
“Moja ya maeneo yaliyopuuzwa katika nyanja hii ni Fiqhi ya Usalama, ambayo licha ya umuhimu wake mkubwa katika muundo wa mfumo wa Kiislamu, bado haijapewa nafasi inayostahili katika mitaala ya kielimu na masomo ya hawza.”

Hujjatul-Islam Abidi alibainisha kuwa: “Katika vitabu vya kawaida vya hawza kama vile Sharh Lum‘a, hakuna sura maalumu inayozungumzia masuala ya usalama, ilhali mada hii ni miongoni mwa mambo muhimu sana yanayohitajika katika jamii ya kisasa.”

Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Maarifa ya Qur’ani Tukufu, akitolea ushahidi kutoka Qur’ani, alisema:


“Kinyume na wanavyodhani wengi, mada ya usalama ina nafasi ya kipekee katika Qur’ani Tukufu, kwani zaidi ya aya 500 zinazungumzia moja kwa moja kuhusiana na Amani — idadi ambayo ni kubwa kuliko aya nyingi za hukumu zinazojulikana (Ayāt al-Ahkām).” Akiashiria changamoto mpya za kiusalama, alisema: “Siku hizi maana ya ujasusi na vitisho vya usalama imepanuka zaidi ya kukusanya taarifa pekee; hata mipango ya kudhoofisha mifumo ya usimamizi au kupotosha vipaumbele vya nchi ni miongoni mwa aina hatari za vitisho vya kiusalama vinavyohitaji uchambuzi wa kina wa kifiqhi na majibu sahihi.”

Mwalimu huyo wa ngazi ya juu wa hawza, akitoa mifano ya masuala mapya ya kiusalama kama vile hukumu zinazohusu operesheni maalumu za kijeshi, upelelezi, kukamata watu katika maeneo matakatifu, na vigezo vya uteuzi wa watumishi wa serikali, alisisitiza:


“Ni wajibu kwa maulamaa na watafiti wa hawza kuingia kwa kina katika uandishi wa Fiqhi ya Usalama kama sehemu muhimu ya Fiqhi ya Mifumo (Fiqh al-Nidhāmāt).”

Mkurugenzi wa Kitengo cha Falsafa katika Chuo Kikuu cha Qom alihitimisha kwa kusisitiza haja ya kupanga mikakati ya kuzalisha elimu na kutoa suluhisho la kifiqhi linalingana na mahitaji changamano ya mfumo wa Kiislamu katika nyanja ya usalama, sambamba na miongozo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika tamko la Hawza inayoongoza na bora.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha